0
Image result for mvua jangwani darMvua iliyoyesha kwa saa kadhaa jijini Dar es Salaam imeacha maafa kwa wakazi waishio pembezoni mwa bonde la mto msimbazi ambapo nyumba nyingi tu zimejikuta zikizingirwa na maji huku wengi wakikosa makazi.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa saa chache tu na kutikisa katika baadhi ya maeneo kadhaa ya kiwemo ya Tandika, Kimara na Vingunguti, ilijikuta ikipeleka maafa kwa wakazi wanaoishi pembezoni mwa mto Msimbazi ambao ndio unaopokea idadi kubwa ya maji kutoka katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Wakazi hao waliokumbwa na maafa hayo wameieleza ITV kuwa wamekwisha kuzoea madhira hayo na kwamba kwao si mageni.

Katika mabonde ya Msimbazi na Jangwani ambayo nyumba nyingi zimekwisha kupigwa X, wakazi wa maeneo hayo wanasema hakuna namna wanavyoweza kuzikwepa nyumba.

Miundombinu katika miji mikubwa kama Dar es Salaam imekuwa ikitajwa kutokuwa rafiki hasa zinaponyesha mvua kubwa huku pia lawama zikielekwa kwa wananchi ambao bado wameendelea kukaidi mamlaka husika ambazo zimekuwazikiwataka kutokuishi ndani ya mabonde ya maji.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top