Papa mdogo ameokowa kutoka kidimbiwa cha kuogelea nchini Australia mbele ya waogeleaji waliokuwa wamepigwa na butwaa.
Hata hivyo Papa huyo hakuonekana kuwa hatari kwa sababu alikuwa bado mdogo.
Watoa huduma kwa wanyamapori walimshika Papa huo mwenye urefu wa futi 3 wakitumia wavu kabla ya kumrejesha habarini.
Haijulikani n kwa njia gani papa huyo aliingia katika kidimbwi hicho cha kuogelea lakini wenyeji wanadai kuwa huenda alisombwa na mawimbi makali kutoka habarini.
"Papa huyo alifanikiwa kujificha kutoka kwa waogeleaji," alisema mama mmoja.
Rita Kluge, ambaye alichukua picha ya papa huyo anasema alionekana kuwaogopa watu zaidi kuliko vile watu walikuwa wakimuogopa.
Hakuwa tisho kwa waogeleaji lakini papa kawaida huwa hatari wanapokuwa wakubwa.
Familia hiyo ya samaki hula samaki wengine na hupatikana sana bahari za Australia.
Post a Comment
karibu kwa maoni