Nahodha na mkufunzi wa zamani Liverpool Ronnie Moran amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83.
Moran alichezea klabu hiyo mechi 379 kati ya 1952 na 1966.
Alikuwa mfanyakazi aliyehudumia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi alipostaafu 1999.
Alijiunga na benchi la wakufunzi Liverpool mwaka 1966 na mara mbili alihudumu kama meneja wa muda - baada ya Kenny Dalglish kujiuzulu 1991 na Graeme Souness alipofanyiwa upasuaji wa moyo 1992.
Mwanawe wa kiume amethibitisha kwamba alifariki mapema Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Alihudumu chini ya mameneja tisa tofauti alipokuwa benchi la kiufundi.
Aliwaongoza Liverpool fainali ya Kombe la FA wanjani Wembley mwaka 1992 akiwa meneja wa muda meneja wao Souness alipokuwa anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni