Lile shindano la kuwatafuta wanafunzi wenye vipaji katika shule za sekondari mjini Babati lililoanza tarehe 18 march mwaka huu limefikia patamu.
Shindano hilo limeandaliwa na Manyara Fm Radio na kupewa baraka zote na ofisi ya mkurugenzi wa mji wa Babati.
Jumamosi hii hapa itakuwa ni fainali kwa ajili ya kuwapata washindi katika kuimba,kucheza mziki na kuigiza ambao watapata nafasi ya kutembelea mbuga ya taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara kujionea wanyama mbalimbali katika hifadhi hiyo maarufu hapa nchini.
Fainali itafanyika katika ukumbi wa redio Manyara Fm ulipo kona ya Nakwa bara bara ya kuelekea mkoani.
Viongozi watakaohudhuria fainali hizo ni pamoja na mbunge wa jimbo la Babati mjini Pauline Gekul,Mkurugenzi wilaya ya Babati vijijini Hamisi Malinga,Mkurugenzi wa mji wa Babati mjini Fortunatus Fwema na wengine.
Wadhamini bado wanaruhusiwa kuja kutangaza biashara zao wakati huu wa mashindano haya ikiwemo ligi inayoanza jumamosi tarehe 25 march MANYARA FM SUPER CUP itakayofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Harambee.

Post a Comment
karibu kwa maoni