Simba wamemaliza mapumziko ya siku mbili na sasa wataanza mazoezi kesho jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Simba walipewa mapumziko ya siku mbili baada ya kurejea wakitokea Arusha.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally 'Gazza' amethibitisha kikosi chake kuwa kitaendelea na mazoezi kesho.
"Tutaanza mazoezi kesho, unajua tumekuwa na ziara mikoani pamoja na kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Madini.
"Kumbuka mikoani tulikuwa tukisafiri kutoka hapa, kwenda kule, hivyo wachezaji walichoka. Wakapewa mapumziko.
"Lakini tunarejea tena mazoezini kuendelea na programu ya mwalimu," alisema.
Simba ilikuwa ziarani Dodoma na Arusha ambako pia ilicheza mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Madini.
Post a Comment
karibu kwa maoni