0
TANZANIA imepangwa Kundi B katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zitakazofanyika nchini Gabon kuanzia Mei 14 hadi 28, mwaka huu.
Katika kundi hilo, Serengeti Boys imepangwa na Angola, Niger na Mali ambayo hata hivyo imefungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), baada ya Serikali yake kuwafukuza viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo (FEMAFOOT). 
Kundi A lina timu za wenyeji Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana na ikumbukwe timu mbili za juu kila kundi zitafuzu moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia za U-17 nchini India baadaye mwaka huu.

Gabon imechukua nafasi ya Madagascar kuandaa fainali hizo, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) chini ya Rais wake zamani, Issa Hayatou wa Cameroon kusema nchi hiyo haikukidhi vigezo vya kuandaa mashindano hayo.
Hata hivyo, hiyo ilihusishwa na upinzani wa Hayatou na Mkuu wa soka ya Madagascar, Ahmad Ahamd ambaye jana alifanikiwa kushinda Urais wa CAF akimuangusha kigogo huyo wa Cameroon aliyedumu kwa miaka 29.
Na Tanzania ikachukua nafasi ya Kongo Brazzaville baada ya wapinzani hao kumtumia mchezaji aliyezidi umri na wakashindwa kumuwasilisha kwa vipimo zaidi ya mara tatu walipohitajiwa na CAF na kufanya hivyo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top