0
TANGAZO  KUTOKA MAGUGU RANGERS KWA WADAU WA MICHEZO.
Ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Manyara  inaanza kutimua vumbi leo March 11. 2017 I katika viwanja tofauti mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa  MARFA Shabani Gwandu amesema kila kitu kimekamilika katika vituo vyote vitatu vya Mererani yenye  timu saba,Babati timu sita pamoja na kituo cha Katesh katika chuo cha VETA  Nangwa timu saba.
Jumla ya timu zinazoshiriki ni 20.
Gwandu amevitaka vilabu vitanavyoshiriki katika ligi hiyo kujiaandaa vyema ili kuonyesha ushindani.
Mechi ya ufunguzi katika kituo cha Babati uwanja wa Kwaraa itakua kati ya Shark Boy dhidi ya Home Boys saa 8:00 mchana,Gallapo Parish dhidi ya MAGUGU Rangers saa 10:00 jioni.
Kituo cha Katesh kutakuwa na michezo miwili watakutana Mrara dhidi ya Young Boys saa 8:00 mchana huku Usalama ikiivaa Morning Star saa 10:00 jioni wakati kituo cha Mererani BCBG wanavaana na Firestone saa 8:00 mchana na mchezo wa pili utapigwa saa 10:00 jioni kati ya Redstart na Nyanza.
Magugu Rangers Fc kutoka Babati imewataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi eo kuishabikia timu hiyo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top