0
Rais Magufuli alifanya mazungumzo na rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein
Image captionRais Magufuli alifanya mazungumzo na rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein
Rais wa Tanzania John Maguful, leo hi amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein kwenye Ikulu mjini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na waziri wa nishati na madini Sospeter Mwijarubi Muhongo, kaimu mkurugnezi mtendaji wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi Kahitwa Bishaija na meneja mwandamizi wa fedha wa TANESCO bwana Sadock Mugendi.
Wakati huo huo waziri wa nishati na madini Sospeter Mwijarubi Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme, baada ya serikali ya mapinduzi Zanzibar kuanza kulipa deni inalodaiwa na TANESCO.
Prof. Muhongo alisema kuwa Zanzibar imeanza kulipa kiasi cha shilingi bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.
Aidha Prof Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO, kulipa madeni katika kipindi cha siku 5 zilizobaki kwa kuwa wasipolipa watakatiwa umeme
Rais wa kisiwa cha Zanzibar Ali Mohamed Shein
Image captionRais wa kisiwa cha Zanzibar Ali Mohamed Shein

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top