0
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira  Mjini Babati {BAWASA} limepanga kutumia maadhimisho ya 29 ya wiki ya maji mwaka huu kutoa elimu,kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika ofisi zao zilizopo bara bara ya kuelekea mkoani.
Utaratibu huu umelenga kutoa mwanya kwa wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka BAWASA kupata Elimu ya Huduma ya Maji  na kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukaribu zaidi kati ya BAWASA na wateja wake.

Mkurugenzi wa BAWASA Eng Iddy Yazidi Msuya ameiambia Manyara Fm kuwa katika wiki nzima hii ya maji wametoa ofa maalum kwa wateja waliokatiwa maji kwa kushindwa kulipia wamewaondolea adhabu hiyo hivyo watalipia kiasi kidogo kwa muda huu ili waendelee kupata huduma ya maji lakini akasisitiza kuwa watahitajika kulipa deni wanalodaiwa kwa awamu mpaka kukamilisha.
Amesema kwa sasa BAWASA inahudumia vijiji vya Himiti na Bonga na wanao mpango wa kufikisha huduma katika kijiji cha Singu.
Zoezi la kupokea kero na malalamiko kwa waanchi linaendelea katika ofisi zao hadi siku ya kilele za kwa wananchi wengi kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa utatuzi.

Aidha katika wiki hii ya maji  BAWASA imendaa Bonanza la michezo katika mpira wa miguu  na mshindi atakabidhiwa zawadi katika kilele cha maadhimisho hayo tarehe 22 mwezi huu.
Maadhimisho ya wiki ya Maji yameanza rasmi  Machi 16 na yanatarajiwa kufika kilele Machi 22 mwaka huu yakibeba kauli mbiu ya “MAJISAFI NA MAJITAKA- PUNGUZA  UCHAFUZI YATUMIKE KWA UFANISI”.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top