Amezungumza hayo wakati akikabidhi vifaa vya maabara kwenye kituo cha afya Mamire vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million nane 8.
Kati ya hizo milioni 2.2 ni vifaa vya maabara na million 6.7 za ujenzi wa maabara nguvu za wananchi na zingine kutoka kwa wafadhili Pharmaccess international Pamoja na mfuko wa Bima ya afya iliyoboreshwa iCHF.
Mpaka sasa mradi huu wa ICHF iliyoboreshwa imesaidia hospitali na vituo vya afya kupata matibabu ya uhakika Kwa vipimo vya kisasa pamoja dawa kupatikana kwa wingi.
Kwa mujibu wa Meneja ICHF mkoa wa Manyara Hance John Mwankenja lengo lao mpaka kufikia June mwaka huu wakazi wa Manyara asilimia 50 wawe wamejiunga na mfuko huu wa Bima ya afya iliyoboreshwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni