0
Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafary Mwanyemba ameng’olewa kwenye wadhifa kwa madai ya kusaini mkataba wa kuchimba visima vya maji katika kata ya Zuzu kinyume na sheria.

Maazimio hayo yamefikiwa leo na kikao maalum cha baraza la madiwani kilichokutana kwa ajili ya kupokea taarifa ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafary Mwanyemba zikiwemo za upotevu wa sh. 31 milion ambazo hazijulikani zilipokwenda.

Hata hivyo katika taarifa ya tume ya uchunguzi iliyokuwa ikiongozwa na afisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Dodoma Cosmas Kanyika ilibainika kuwa fedha hizo zililipwa kwa mkandarasi wa mradi huo Kallago Interprises kwa ajili ya kuchimba visima vya maji ambapo hata hivyo baada ya kushindwa kuifanya kazi hiyo alishindwa kuirudisha fedha hiyo.

Amesema mkandarasi huyo alitumia kiasi cha sh. 18 milion kwa ajili ya kuchimba visima viwili katika Kata ya Zuzu lakini hata hivyo visima hivyo havikuweza kutoa maji mpaka sasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya tume ya uchunguzi iliyoundwa baada ya ubalozi wa Japan nchini kutembelea mradi huo na kuona matunda yaliyokusudiwa hayajapatikana walitaka fedha zilizotolewa kwa mkandarasi zirejeshwe ambapo Mstahiki Meya Mwanyemba alilazimika kurejesha fedha hizo kiasi cha sh. 30 milion baada ya kuombwa kufanya hivyo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde ili kunusuru mradi huo usiondolewe kwa wananchi wa kata ya Zuzu.

Hata hivyo tume hiyo haikuonyesha mahali popote ambapo Mstahiki Meya Mwanyemba alihusika na utengenezwaji wa mkataba huo licha ya kuusaini tu na kusema kuwa tuhuma zote hazikuwa za kweli dhidi yake baada ya kuwahoji madiwani wanaompinga, madiwani wanaomuunga mkono na watumishi wa Manispaa ya Dodoma.

Lakini hata hivyo baada ya taarifa ya tume ya uchunguzi iliyoundwa kusomwa madiwani walitaka kura za siri zipigwe na ndipo wengi wao waliposema kuwa hawana Imani na Mstahiki Meya huyo.
Sakata la kutokuwa na Imani na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma liliibuliwa na baadhi ya madiwani wa Manispaa hiyo baada ya Meya huyo kusaini mkataba wa kuchimba visima virefu vya maji katika Kata ya Zuzu uliokuwa na thamani ya sh. 122 milion kinyume na taratibu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top