KUKAMILIKA barabara ya Bonga mkoani Manyara hadi Mela mkoani Dodoma yenye urefu wa kilomita 88.8 umeelezwa kuwa utafungua fursa za uwekezaji na biashara kwa wazawa wa mji wa Babati na vitongoji vyake.
Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika Oktoba 1, 2017.
Akizungumza na JOHN WALTER BLOG ofisini kwake Meneja wa TANROADS Mkoa wa Manyara Eng. Bashiri R. Rwesingisa, amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya barabara.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha wananchi wanaoishi mabondeni akiwataka kuhama ili kuepuka adha inayoweza kuwapata akitolea mfano wananchi wa kijiji cha Gendi Babati.
Mradi mwingine ni wa bara bara mkoani Manyara unaohusisha ujenzi wa kilometa 17.8 kutoka Bereko hadi Bonga kazi inayotekelezwa na Mkandarasi M/S China Railway Seventh Group Ltd kutoka China.
Kipande hicho kinafadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Misaada la Japan(JICA) na utagharimu jumla ya shilingi bilioni 83.370.
Amesema mradi huo ni utekelezaji wa miradi miwili ya kitaifa hadi robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2017 inayoendelea mkoani hapa ukifuatiwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya KIA-Mirerani kwa kiwango cha lami kwa km 26 utakaogharimu jumla ya shilingi bilioni 32.214 ambapo unatarajiwa kukabidhiwa mwezi april 12/ 2017.
Rwesingisa alifafanua kuwa sambamba na ufunguzi wa barabara pia itarahisisha mawasiliano ya kiutendaji baina ya mikoa jirani ya Dodoma ambapo ni makao makuu ya nchi na kupunguza kwa mwendo mrefu kwenda mikoa ya Dodoma na Dar es Salam.
Post a Comment
karibu kwa maoni