Mafundi magari na uchomeleaji vyuma Mkoani Manyara wameanzisha Chama chao ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kuanzisha viwanda vidogo na kuwa na maeneo maalum ya kufanyia shughuli zao.
Wakizungumza na TBC, Mafundi hao wamesema wamefikia uamuzi huo ili kuunga mkono jitihada za Rais Dokta John Magufuli za kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuwa na nguvu ya kiuchumi.
Naye Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa BABATI KENETH SHEMDOE amesema changamoto zinazowakabili mafundi hao zitatafutiwa ufumbuzi kupitia chama chao.
Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Manyara Venance Msafiri amesema chama hicho kitawawezesha kutambulika na kufanya kazi na Taasisi za umma.

Post a Comment
karibu kwa maoni