Mchungaji
wa kijiji kimoja huko zimbabwe Pastor Jonathan Mthethwa ametafunwa
vizuri na mamba watatu alipokuwa akijitutumua kutembea juu ya maji Kama
yesu katika mto MPUMALANGA au kwa jina maarufu MTO MAMBA kutokana na wingi wa mamba katika mto huo.
Alikuwa anafanya majaribio ya imani(DEMO) aliyowafundisha waumini wake kanisani....
Shemasi aliyehojiwa anashangaa kwa nini aliliwa maana kabla alifunga na kuomba wiki nzima...
Mashuhuda
wanasema alitembea ndani ya maji kama mita 30, alipotaka kuanza kupanda
ili aanze kutembea juu ya uso wa maji ndipo yalitokea mamamba makubwa
matatu na kumtafuta na kumkatata vipande huku mwili wote ukiishia kwenye
matumbo ya watafunaji hao...
Waumini
Muwe makini na Wachungaji wenu, Leo kaenda yeye kesho anaweza kuibuka
mwingine TZ akawaambia kanisa zima litembee juu ya mto ruvu ile sehemu
yenye mamba na viboko wengi kama mazoezi ya Imani. Au kama mafunzo ya
vitendo baada ya kufundishwa Theory/Nadharia za kiimani kanisani...
Post a Comment
karibu kwa maoni