0
Jumamosi ya tarehe 23 septemba Mwaka huu Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli


atawatunuku nishani maafisa mbalimbali wa jeshi la wananchi wa Tanzania
(JWTZ) zoezi linalotarajiwa kufanyikia katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini ARUSHA.

Kwa mujibu wa taratibu za kijeshi, Mtanzania yeyote
anayesomea nje ya nchi akihitimu inabidi arudi nchini ili atunukiwe kamisheni
na Amiri Jeshi Mkuu.





Chuo cha Kijeshi kilianza mwaka 1969, Kurasini jijini Dar es
Salaam kutokana na mahitaji ya mafunzo yanayozingatia maadili ya Kitanzania, na
baadae kilihamishiwa Monduli, Arusha mwaka 1976.


Kwa kuthamini ujio wa rais katika jiji hilo mkuu Wa mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo amewakaribisha wakazi wa mkoa huo kufika na kusikiliza
kitachozungumzwa na Mheshimiwa rais Magufuli.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top