0
Jana Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia mkusanyiko wa watu walioongozwa na Meya wa Arusha kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba kwenye ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.
Tukio hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Madiwani, Waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa dini (Wakristo na Waislamu) lilifanyika kwenye eneo la shule hiyo ya Lucky Vicent ambapo wakati wakiendelea kuzungumza wakiwa gorofani ghafla waliona Polisi wamefika kwa spidi na kusema watu wote wako chini ya ulinzi.
Baada ya hapo Polisi waliwakamata na kuondoka nao wote wakiwemo Waandishi wa habari wapatao kumi ambapo baada ya kufika kituo cha kati cha Polisi, Waandishi hao waliachiwa huru huku Polisi wakiwaambia hawana shughuli nao bali waliwapa lift tu kutoka kwenye eneo la tukio.
Kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika dakika chache baadae, Polisi walisema aliyeamuru Waandishi kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni hakufahamu kwamba hao ni Waandishi na kwamba Wanahabari hao hawana kosa lolote na ndio maana waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.
Taarifa zaidi kuhusu viongozi wa dini, Meya na Madiwani ambao bado wameendelea kuhojiwa na Polisi zitakujia muda sio mrefu

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top