0
Wakazi wa Babati mkoani Manyara wakizubgumza na redio Manyara fm wamewataka wafanyabiashara kushusha bei za bidhaa katika msimu huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Wamesema kuwa wanashangazwa kuona bidhaa zikiendelea kupanda wakati gharama za nauli hazijapanda.
Nao wafanyabiashara wameeleza kuwa kinachowafanya wao kupandisha bei za bidhaa ni kutokana na mzalishaji kumuuzia bei ya juu hivyo analazimika kupandisha walau apate faida.
WAKATI BEI ZIKIPANDA HUKU BARA VISWANI ZANZIBAR WATANGAZIWA NEEMA MSIMU HUU WA MWEZI MTUKUFU.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itapunguza  kodi  kwenye bidhaa muhimu zitakazotumika katika  mwezi mtukufu wa Ramadhani  ili kuwaondolea usumbufu wananchi katika kipindi hicho cha kutekeleza ibada tukufu ya funga.
Akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje Waziri wa Fedha na Mipango Dr.Khalid Salum Mohamed amesema lengo la kuwapunguzi kodi wafanyabiashara  ni kuwapa unafuu zaidi  wananchi  na waumini ili waweze kumudu gharama za mwezi huo mtukufu.
Hata hivyo  Dr.Khalid amesema endapo unafuu huo uliotolewa na serikali  kwa wafanyabiasha wakiutumia vibaya serikali haita sita kuwachukulia hatua za kisheria kwani lengo ni kuwanufaisha wananchi hasa wanyonge katika kipindi cha ramadhani kununua bidhaa wanayoihitaji bila usumbufu.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top