Mbunge
Jakuh Hashim Ayoub amemuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mwezi
mtukufu wa Ramadhan na kuna tatizo la sukari huku wananchi wakiwa na
uhitaji na kwamba hivi sasa zipo tani 100,000.
Amemweleza Majaliwa kuwa sukari iliyoagizwa kwa watu waliopewa vibali vya sukari itakuwa imekwisha wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapoanza.
Akijibu swali hilo Majaliwa amesema kuhusu kupungua kwa sukari na mahitaji yake nchini kuwa Serikali iko macho na itafanya jitihada za kupata mahitaji yote.

“Mahitaji
ya sukari nchini ni tani 420,000 lakini kwa sasa tunazalisha tani
320,000 hivyo mwaka huu Serikali imeagiza tani 80,000 na tayari tani
35,000 zimeshaingizwa nchini,”amesema Majaliwa.
Hata
hivyo, Majaliwa amewasihi wafanyabiashara kushusha bei ya sukari
waliyoipandisha kwani Serikali inashirikiana nao ili kuweza kuweka
mazingira rafiki kwa wananchi.
Post a Comment
karibu kwa maoni