0

Responsive imageBaadhi ya Mbwa wanaozurura mitaani katika mji wa Babati waliouwawa kwa kupigwa risasi na Idara ya mifugo ya Halmashauri ya mji wa Babati.
 
  Jumla ya Mbwa 347 kati ya zaidi ya 3600 wanaozurura mitaani katika mji wa Babati  mkoani Manyara wameuawa kwa kupigwa risasi na Idara ya mifugo ya Halmashauri ya mji wa Babati.
Mbwa hao wameuawa katika kipindi cha mwezi Mei na Juni mwaka huu kufuatia ongezeko kubwa la Mbwa wanaozurula mitaani na kutishia usalama wa Wakazi wa mji wa Babati ambapo katika kipindi cha kuanzia Junuari hadi mwishoni mwa Mei mwaka huu jumla ya watu 264 waling’atwa na Mbwa.
Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya mji wa Babati Dakta Fatuma Mkombozi amesema zoezi hilo ni endelevu mpaka watakapowateketeza mbwa wote wanazurura mitaani na kutishia amani.
Kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka 2016 mji wa Babati unakadiriwa kuwa na Mbwa 4,923 ambao kati yao Mbwa 3,693 sawa na asilimia 75 wanazurula mitaani na asilimia 35 ya wanaozurula mitaani hawana wamiliki.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top