0
Responsive imageWaziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amesikitishwa na hali duni ya maisha ya jamii ya Wahadzabe, Watindiga na Watatoga wanaoishi katika Bonde la Yaeda Chini Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.

Prof Maghembe amesema haiwezekani jamii hiyo ikaendelea kuishi kwa kula Unga wa Mibuyu, Mizizi na Wanyamapori wakati kila siku watalii wanaenda katika bonde hilo kuangalia jamii hiyo.

Katika risala yao iliyosomwa na Daines Naftari mwanajamii ya Wahadzabe wamesema Majangili wamesababisha kutoweka kwa Wanyamapori wanaowatumia kama kitoweo chao na ukame ukitajwa kusababisha njaa

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top