0
Image may contain: 1 person
UPDATE:Majira ya saa moja usiku jana milio ya mabomu ya machozi ilisikika mitaa ya Nakwa Babati Manyara huku hali iliyowafanya wakazi wa mtaa huo kuingiwa na hofu kubwa.
Wakazi wa mtaa huo walidai kuwa ni polisi ndio waliopiga mabomu hayo kutawanyisha vikundi vya kihuni.
Leo Kamanda wa polisi mkoani Manyara Francis Jacob Masawe amekanusha kutokea kwa mlipuko huo huo huku akisema 'kama wamesikia mabomu yakilia wajiulize na waendelee kujiuliza kipi kimesababisha hali hiyo kutokea'.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top