Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam jana , Mabawa alisema kuwa lengo la
kampeni hiyo ni kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupigania
rasilimali za wananchi wanyonge na masikini na kuunga mkono juhudi
anazozifanya na hivyo kampeni hiyo inahamasisha yeye kubaki katika
msimamo wake pasipo kusikiliza maneno ya watu.
“Napinga
kwa nguvu zote, kama nilivyokwisha kufafanua toka mwanzo ,kampeni ya
‘Magufuli Baki’ ina lengo la kumtia moyo Rais Magufuli na kumwomba abaki
katika msimamo wake wa kutetea maskini, wanyonge na kupigania
rasilimali za taifa letu,
“Nirudie
tena wito wangu kwamba nitazunguka nchi nzima kwa gharama zangu kupata
fursa ya kuwasikiliza wananchi kupitia kampeni yangu inayojulikana kwa
‘Magufuli Baki’ kuhakikisha wananchi wanatoa maoni yao juu ya rais
kuendeleza msimamo wake wa kiutendaji na sitavunjwa na propaganda za
baadhi ya vikundi vinavyonikejeli mitandaoni pasipo kuthamini maendeleo
anayoyafanya,” alisema.
Aidha
alieleza kwamba toka aitangaze kampeni yake kumekuwa na tabia kwa
baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao hutoa lugha za maudhi na kejeli
kwa baadhi ya Watanzania wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais
Magufuli na serikali yake.
Alisema
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
ibara ya 18 kifungu kidogo cha (1) na (2) kinatupa haki na fursa ya
kutoa maoni na kueleza fikra zetu, hivyo amewaomba wanasiasa wasitumie
kifungu hicho cha katiba kukivunja kwa kutoa maoni yenye kuudhi na
kejeli, kwa hiyo, alisema, kitendo cha kushambuliana kwa maneno makali
ni kosa kisheria.
Alisema
kampeni aliyoianzisha itaweza kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao
ambayo yatasambazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya
kijamii kuanzia mwezi ujao.
Post a Comment
karibu kwa maoni