Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, imeendelea kupata
hati safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini
(CAG), kwa mwaka wa saba mfululizo.
Akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya CAG ya mwaka wa fedha
2015/2016, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, aliitaka halmashauri hiyo
kutobweteka baada ya kupata hati safi badala yake waongeze juhudi zaidi. Amesema kuwa, viongozi wa halmashauri hiyo wanapaswa kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakamilishwa kwa wakati na kutekelezwa kwa ubora , kutunza vyema taarifa za fedha ili kuendelea kupata hati safi.
Post a Comment
karibu kwa maoni