UTAFITI uliofanywa na
taasisi ya Twaweza umeonyesha kuwa usalama kwa nusu ya Watanzania
umeimarika katika mwaka mmoja uliopita kwa asilimia 53 ambapo asilimia
37 walisema hali ya usalama imebaki vilevile na asilimia 10 wanasema
hali imekuwa mbaya zaidi.
Utafiti huo umetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, katika mkutano na wadau
uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar, alipofafanua kuwa
matokeo hayo yametokana na utafiti wake uitwao ‘Hapa usalama tu:
Usalama, polisi na haki nchini Tanzania’.
“Muhtasari huu unatokana
na takwimu zilizokusanywa kutoka sauti za wananchi, utafiti wa kwanza
barani Afrika kwenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mkononi.
Ni matokeo na takwimu
zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,805 katika maeneo mbalimbali ya
Tanzania Bara bila kuhusisha serikali ya Zanzibar yaliyofanyika Aprili
mwaka huu,” alisema.
YALIYOMO KWENYE RIPOTI YA TWAWEZA
Post a Comment
karibu kwa maoni