0




Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu leo
amesomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya
dhamana yake.


Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya
uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri.




Mawakili watano wa upande wa Jamhuri
waloshiriki katika kesi hiyo, wameiambia Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo
la jinai Julai 17 mwaka huu katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es
Salaam.




Lissu ambaye alikuwa akitetewa na jopo la
mawakili 20 wakiongozwa na Fatma Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge
huyo pia alisikika akisema, “kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.”




Baada ya
kusikiliza pande zote mbili Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 27 ambapo
hatma ya dhamana ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria
wa Tanganyika (TLS) itakapojulikana.
Lissu
alivalia mavazi suti nyeusi huku ndani yake akiwa amevaa fulana yenye
maandishi ya UKUTA,operesheni hiyo ilipigwa marufuku hivi karibuni na
jeshi la polisi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top