Watu watano wameuwawa kwa kuchomwa moto katika kata
ya Uchama Wilayani Nzega Mkoani Tabora na watu wanaosaidikiwa kuwa ni
Sungusungu huku wakidaiwa wameuliwa kutokana na imani za kishirikina.
Kufuatia Mauaji hayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agreya
Mwanri, amezitaka Kamati za Ulinzi na usalama ngazi ya Mkoa na ile ya Wilaya ya
Nzega kusitisha shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na sungusungu katika kijiji
hicho.
Mwanri amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya
sungusungu hao kutekeleza mauaji hayo ya watu watano ambao wote ni wanawake
wakituhumiwa kuwa ni washirikina.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa katika kuendelea
kuchunguza tukio hilo jeshi hilo linawashikilia baadhi ya viongozi wa kijiji hicho
ili kuweza kubaini waliotekeleza tukio hilo.
Post a Comment
karibu kwa maoni