Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amebadilikia Mbunge wa Jimbo la Morogoro
Mjini Mh Aziz Abood na kumtaka arudishe viwanda mbalimbali ambavyo
alibinafsishiwa na serikali kama ameshindwa kuviendesha.
Rais Magufuli amesema hayo leo
alipokuwa Morogoro mjini na kuwataka watu waliobinafsishiwa viwanda na serikali
mkoani humo na wameshindwa kuviendesha wavirudishe kwa serikali ili serikali
iweze kuwapa watu wengine ambao wataweza kuviendesha.
“Ninarudia
wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro
ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye
alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili
tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi
kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu” amesisitiza
Mhe. Rais Magufuli.
Mbali na hilo Rais Magufuli
amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro SACP - Ulrich Onesphory Matei
kuhakikisha askari Mgambo hawawasumbuli wafanyabiashara wadogo wadogo na
amewataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri
unaandaliwa kwa ajili yao.
Rais Magufuli wakati akiwa katika
ziara mkoani Singida aliweka wazi kuwa yeye anauchukua sana ubinafsishaji na
kusema ndiyo umeturudisha nyuma na kuharibu mipango mizuri ambayo alikuwa nayo
Mwalimu Nyerere, huku akitolea mfano viwanda kadhaa ambavyo vipo Morogoro na
vimeshindwa kuendelezwa na majengo yake kugeuka magodauni ya watu.
Post a Comment
karibu kwa maoni