0
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga  ameagiza Mkuu wa Shule ya Sekondari Siday Denis Lukumay akamatwe na kuwekwa rumande akidaiwa kumruhusu mwanafunzi Yuditha Mohammed kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
DC Mofuga ameeleza kuwa Mkuu huyo aliruhusu mwanafunzi kusoma akiwa mjamzito na kuendelea na masomo pia baada ya kujifungua huku kitabu cha mahudhurio akionekana kuhudhuria kama kawaida.
>>>”Anaruhusu mjamzito kusoma akiwa shuleni. Ameenda kujifungua bado mahudhurio yanaonesha bado alikuwa shuleni. Badala ya kutafuta wahalifu waliompa mimba mwanafunzi, yeye anamuweka shuleni.” – DC Mofuga.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top