0
Baada ya operation ya kuondoa mifugo katika Hifadhi na Mapori ya Akiba May 2017 ambapo Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheruka alipotea porini kwa siku nzima, imeanzishwa operation nyingine kuondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na uchafuzi wa mazingira.
DC Mheruka akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo, ameanzisha operation nyingine ya kuondoa wananchi waliovamia katika vyanzo vya maji na kuharibu mazingira ambapo wakiwa katika kijiji cha Chabuhora katika Kata ya Nyakabanga jirani na pori la Kimisi, wawakuta wananchi waliovamia vyanzo vya maji na kuweka makazi ya muda katika eneo lenye ekari 15 na kuanzisha shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, kukata miti ovyo, kuchoma mkaa pamoja na uwindaji haramu.
Kufuatia waliamua kuteketeza makazi ya wananchi hao na kuwataka warudi katika makazi yao ya zamani ikiwa ni pamoja na kuwaagiza Watendaji wa Kitongoji hadi Wilaya kusimamia zoezi hilo kuhakikisha hawarudi katika maeneo hayo kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top