0






MGOMO wa kutohudhuria mahakamani uliotangazwa na Rais wa Chama cha Mawakili
Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, umepingwa na kukosa kuungwa mkono baada ya
mawakili kujitokeza kwa wingi mahakamani jana huku wakieleza kuwa ni wazo la
mtu mmoja na kwamba huenda wanaogoma hawana kesi katika siku hizo mbili.



Lissu aliwaeleza waandishi wa habari Jumapili kuwa Baraza la Uongozi la TLS
limetangaza mgomo wa siku mbili, kupinga uharibifu uliotokana na mlipuko kwenye
Ofisi za Kampuni ya Mawakili ya Immma iliyoko Upanga katika Manispaa ya Ilala
jijini Dar es Salaam.



Lakini jana, mawakili walikuwapo mahakamani kama walivyoshuhudiwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam uwepo wa mawakili wachache ambao
ni wakongwe huku idadi kubwa ikiwa ni ya mawakili wapya ambao huenda waliingia
kwenye tasnia hiyo hivi karibuni.



Kituo hiki kilifika ofisi za mwenyekiti wa mawakili mkoa wa Manyara zilizopo
Babati Mjini Wakili Tadey Lister na kutoa maoni yao baada  ya agizo la TLS chini ya Lissu, ambaye pia ni
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), kuwaagiza kugoma kwa siku mbili; jana na
leo.



Mkoani Arusha, mawakili wanachama wa TLS walisema hawawezi kuunga mkono
mgomo huo kwa kuwa ni batili na unakiuka maadili ya taaluma hiyo. Wakili Pares
Parpay alisema haungi mkono mgomo huo kwa sababu ameingia mikataba na wateja
wake ambao ni wananchi na tayari ameshalipwa mamilioni ya fedha kwa kazi hiyo
hivyo kugoma ni kumsaliti mteja wake.



Alisema ni aibu kwa mtu kama yeye kuamua kutoka usingizini na kuunga mkono
mgomo wa kutokwenda mahakamani kwani mteja wake atashindwa kumwelewa na kauli
za namna hiyo zinapaswa kuangaliwa upya kwani zinaweza kutuingiza mahali pabaya
bila ya sababu za msingi.



“Sisi kazi yetu ni kuwatetea wateja wetu na kuunga mkono mgomo ni kumwonea
mteja wangu aliyenipa pesa nyingi kufanyia kazi mahakamani kwa niaba yake,”
alisema na kuitaka TLS kuviacha vyombo vya usalama kufanya kazi yake kikamilifu
ili wahusika wachukuliwa hatua kali.



Naye Edmund Ngemela alipinga kuunga mkono mgomo na kueleza kuwa kufanya
hivyo ni kuidhalilisha taaluma ya kuwadhalilisha wateja walioingia nao mkataba
wa kufanya kazi mahakamani. Alisema mgomo ulipaswa kushirikisha pande zote
ikiwemo Mahakama na kama hilo halikufanyika basi mgomo huo ni batili.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top