WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametembelea mradi wa
kuunganisha matrekta ya Ursus, uliopo Kibaha mkoani Pwani na kusisitiza
kuwa Serikali imedhamiria kuendeleza kilimo nchini ili kukuza sekta ya
viwanda.
Tayari
Matrekta 204 yenye uwezo wa HorsePower 50 yamekwisha unganishwa
yakisubiri kuuzwa kwa watumiaji hatua ambayo Dkt. Mpango amesema
itaongeza tija katika kilimo na kukuza ajira hususan kwa kundi kubwa la
vijana.
Ameahidi
pia kuwa Serikali itayafanyiakazi haraka maombi ya Shirika la Maendeleo
la Taifa NDC la kutaka kupata kibali cha kuajiri zaidi ya wafanyakazi
90 watakaohusika na mradi huo pamoja na kutoa shehena ya Matrekta 267
yaliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili yaweze kuuzwa kwa
wananchi kuendeleza kilimo.
Kwa
upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo la
Taifa-NDC, Mhandisi Adam Mbura, amesema mradi huo utahusisha pia
uanzishwaji wa vituo vinane katika kanda mbalimbali kwa ajili kuuza
matrekta, zana na vifaa vingine pamoja na kutoa huduma kwa wateja.
Amesema
kuwa kukwamuliwa kwa makontena 64 yaliyokwama bandarini yakiwa na
matrekta hayo 267 pamoja na vipuri vya kuunganisha Matrekta hayo pamoja
na baadhi yaliyopo katika eneo la Mradi la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani,
kutawezesha kukamilisha haraka kwa kazi hiyo.
Baadhi
ya vijana wanaofanyakazi katika mradi huo wamesema kuwa wamenufaika na
ujuzi wanaoupata kutoka kwa wataalamu wa ufundi kutoka nchini Poland na
kuahidi kuuendeleza ujuzi huo kwa vijana wenzao ili mradi huo uweze kuwa
na manfaa kwa kutatua changamoto mbalimbali za kiufunsi zitakazokuwa
zikiwakabili wakulima
Mradi
wa kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, Kibaha Mkoani Pwani
unafadhiliwa na Serikali ya Poland ambapo kiwanda kikubwa cha
kuunganisha matrekta kinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo na yatauzwa
kwa gharama nafuu, kati ya shilingi milioni 38 hadi milioni 42 kulingana
na ukubwa na uwezo wa trekta.
Post a Comment
karibu kwa maoni