Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amelishukuru Shirika la
Maendeleo la Japan-JICA, kwa uwekezaji mkubwa uliofikia kiasi cha
Shilingi trilioni 74.93 katika miradi mbalimbali ya maendeleo hapa
nchini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Dkt.
Mpango ametoa shukrani hizo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Shirika hilo, aliyepo katika ziara ya kikazi hapa
nchini, Bw. Shinichi.
Kiasi
hicho cha fedha kinahusisha ruzuku asilimia 76.0, mikopo yenye masharti
nafuu asilimia 3.8 na usaidizi wa kiufundi asilimia 20.1.
Amemwomba
Rais huyo wa JICA, kuongeza ufadhili kwenye miradi ya nishati ya umeme,
miundombinu, afya, kilimo na uvuvi kusaidia kasi ya Serikali ya Awamu
ya Tano katika kukuza uchumi wa viwanda.
“Sekta
ya viwanda haiwezi kuendelea kama hakutakuwa na uwekezaji mkubwa kwa
upande wa nishati ya umeme pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara”
alisisitiza Dkt. Mpango.
Amesisitiza
pia umuhimu wa Shirika hilo kuisaidia Tanzania kuboresha sekta ya afya
kwa kujenga Hospitali zitakazo hudumia magonjwa makubwa kama ya moyo na
mengine mengi pamoja na kuweka vifaa vya kisasa kwa kuwa Japan inafanya
vizuri katika masuala hayo.
“Eneo
lingine tunaloona ni muhimu ni kusaidia kutoa ufadhili wa masomo ya
ujuzi wa aina mbalimbali kwa vijana wetu ili waweze kusaidia nchi katika
nyanja mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi” aliongeza Dkt. Mpango.
Kwa
upande wake, Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Bw. Shinichi
Kitaoka, ameahidi kuwa shirika lake litaendelea kushirikiana na Tanzania
katika kutatua changamoto zinazokwaza maendeleo yake.
Amesema
kuwa pamoja na kuendelea kusaidia ujenzi wa miundombinu, Shirika lake
litaangalia namna ya kusaidia Sekta ya afya kwa kuboresha lishe kwa
watoto ili kujenga kizazi imara na chenye nguvu.
Bw.
Shinichi Kitaoka ameahidi kwenda kuwahamasisha wawekezaji mbalimbali
kutoka nchini mwake kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa kuna fursa nyingi za
kiuchumi.
Japan,
kupitia Shirika lake la Maendeleo-JICA, inatarajia kutekeleza miradi
mipya maendeleo hapa nchini ukiwemo awamu ya pili ya ujenzi wa barabara
kutoka Moroco hadi Mwenge Jijini Dar es Salaam, utakayogharimu shilingi
bilioni 1.38, ambao mkataba wake utasainiwa majuma mawili yajayo.
Mradi
mwingine ni upanuzi na uboreshaji wa barabara ya kuanzia makutano ya
eneo la Kamata na barabara ya Kilwa, unaotarajiwa kuanza wakati wowote
baada ya masuala ya changamoto za kiufundi kukamilika, utakao gharimu
shilingi bilioni 24.2.
Aidha,
Japan, imefadhili mradi wa ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili
utakaogharimu Dola milioni 269.8 utakapo kamilika huku mradi mwingine
unaoendelea ni ule wa ujenzi wa barabara za juu katika eneo la TAZARA,
Jijini Dar es Salaam.
Kuhusu
biashara kati ya Tanzania na Japani, imeendelea kuimarika ambapo kati
ya mwaka 2015/2016 nchi hiyo imeingiza bidhaa nchini zenye thamani ya
Dola milioni 363.0 hadi kufikia Dola milioni 371, sawa na ongezeko la
asilimia 2.2
Katika
kipindi hicho Tanzania haikufanya vizuri ambapo kiwango cha mauzo ya
bidhaa nje ya nchi kilishuka kutoka Dola za Marekani milioni 229.7 hadi
Dola milioni 138.5 sawa na asilimia 39.7 hali iliyosababishwa na
ushindani mdogo wa wazalishaji wa Tanzania ikilinganishwa na wenzao wa
Japani.
Post a Comment
karibu kwa maoni