0
NA GHAROS RIWA  BUNDA +255768443315/0717646555

Takribani kata zipatazo 30 kati ya 33 zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Bunda  Mkoani Mara zimeshiriki katika uchaguzi wa kuwapata viongozi ndani ya chama cha Mapinduzi CCM hii leo Agost 5, 2017.

Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya hiyo Bwana Mabutu Malima amesema kata ambazo hazikufanya uchaguzi huo ni Kibara, Hunyari na Sazira ambazo zilikabiliwa na changamoto mbalimbali, hata hivyo hakutaja changamoto hizo.

Kufuatia uchaguzi huo Bwana malima ambae pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wailaya na halmashauri kuu wailaya naye kwa mujibu wa wa taratibu za chama hicho ni mjumbe halali wa uchaguzi huo.

mapema asubuhi Bwana Malima katika kata ya kabarimu iliyoko katika halmashauri ya mji wa bunda amejitokeza kwenda kupiga kura, huku baadhi ya wajumbe wa mkutano maalumu wa uchaguzi huo nao wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.

Kupitia Mkutano huo maalumu wa uchaguzi Katibu huyo wa ccm wilaya ya Bunda ametumia muanya huo kuwahutubia wanajumbe wa mkutano huo na wana ccm wote wilayani hapo na kuwataka wajumbe wote kutafuta viongozi wanaokubalika ndani na nje ya chama na siyo wale wanokubalika kwenye kundi la chama hicho pekee kwakuwa wana ccm ni wachache na watu wengi wako nje ya chama hicho.

amesema wachague kiongozi aneshirikiana na wananchi katika shida na raha, pia anaekubalika na asiepandikizi la mtu au kikundi cha watu wenye maslahi yao yaliyojificha.

amesema kuwa wapo waliofanya hivyo mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu  na hatimae majina yao yalikatwa hatimae wakaamua  kundoka nje ya ccm na kwenda kujiunga na upinzani wakidhani kuwa watapata uongozi lakini mpaka leo hawajapata, na kusisitiza  kuwa kamwe hawatapata.

Amesema kuwa chama hicho kwa sasa kimejengwa upya na unapinga mambo yanayoenda kinyume na utaratibu wa chama na hivyo hakitamvumilia mtu yeyote atakae kwenda kinyume na maadili.

Aidha pamoja na kuwaasa wanachama kufuata utaratibu lakini pia amewataka viongozi watakochaguliwa kushika hatamu za uongzo katika awamu hii kuwa washifrahie nafasi zao hizo na kuanza kuwabeza wale waliokoswa kwani inaweza kugundulika kuwa alitumia rushwa na hatimae akapokonywa nafasi yake hiyo.

Hata hivyo katika uchaguzi huo kata zilizokuwa zikizungumzwa zaidi na wadau mbalimbalikuwa zinaweza kuwa na utata ni pamoja na kata ya kabarimu, ambapo uchaguzi wake umefanyikia katika ukumbi wa Mnazi mmoja ulipo mtaa wa Saranga maarufu kama mtaa wa benki, kutokana na uwepo wa vigogo wa halmashauri ya mji huo kuwepo katika mtaa huo.






Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top