0
Mshambuliaji wa kimataifa wa Liverpool, Mmisri, Mohammed Salah, amesema hatoweza kujiunga na Real Madrid kutokana na mchezo ambao si wa kiungwana waliouonesha jana wakati wakicheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Ukraine.

Salah ameeleza kusikitishwa zaidi na tukio la nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos kwa kitendo chake cha kumuumiza mkono na kupelekea kuondolewa nje ya Uwanja baada ya kushindwa kuhimili maumivu.

Mchezaji huyo amesema kitendo kama hicho ni mbinu chafu za kujitafutia matokeo badala ya kucheza mpira ambao unafuata sheria zote 17 za mchezo wa soka.

Kuafuatia rafu iliyopelekea kuumia mkono wake, Salah amesema hataweza kujiunga na timu hiyo ambayo imeonesha nia ya dhati kutaka kumsajili hivyo ataendelea kusalia Liverpool na si kwenda Madrid.

Katika mchezo huo uliopigwa mjini Kiev, ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuweza kubeba taji la tatu mfululizo katika UEFA Champions League.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top