![]() |
Bwana Odinga, 72, alishindwa mwaka 2007 na 2013 |
Utulivu unashuhudiwa nchini Kenya
baada ya kampeni kali wakati nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa siku ya
Jumanne.
Miaka 10 iliyopita zilishuhudiwa
ghasia mbaya nchini humo ambazo hakuna mtu angependa zirudie tena.
Lakini huku kura za maoni kuonyesha
kuwepo kinyanganyiro kikali kati ya rais wa sasa Uhuru Kenyatta na kiongozi wa
upinaani Raila Odinga, kuna hofu kuwa huenda kukawa na matatizo mbeleni.
Kile ambacho hufanyika nchini Kenya
hakihusiani sana ni nani atakuwa mshindi bali vile wale walioshindwa
watachukulia kushindwa kwao.
Mafanikio ya mifumo wa kidigitali ya
tume ya uchaguzi na mipaka yatakuwa muhimu kwa uchaguzi huo kutajwa kuwa wenye
huru na haki.
Ikiwa mifumo hiyo itafeli sawa na
mwaka 2013 kura zitahesabiwa kwa mikono, na katika nchi ambayo imekubwa na
madai ya wizi wa kura bado yule ambaye atashindwa atapinga matokeo hayo.
![]() |
Rais Kenyatta na matumaini ya kuchaguliwa tena |
Mwaka 2013 Raila Odinga alidaia
kuwepo udanganyifu na alipoteza kesi mahakamani.
Wakati huu, akiwa anawania kwa
muhula wa nne na hasa mara ya mwisho, anaweza akaingia mitaani ikiwa atahisi
kuwa kura hizo zimeibiwa.
Kuuliwa kwa meneja wa masuala ya
kompiuta wiki moja kabla ya uchaguzi ni kisa kimezua wasi wasi nchi Kenya
Chris Msando alikuwa akisimamia
mifumo ya eletroniki na alionekana kwenye runinga akihakikishia umma kuwa
mifumo hiyo itafanikiwa na haiwezi kudukuliwa.
Wakati mwili wakae uliokuwa na
majera mabaya ulipatikana kwenye kichaka, madai yaliibuka kuwa kuna mtu alikuwa
anapanga kuingilia kati uchaguzi.
Ikiwa hakuna mgombea atashinda kwa
zaidi ya asilimia 50, basi uchaguzi utaelekea duru ya pili. Lakini kutokana na
kutowepo mgombea maarufu wa tatu hizi inaonekana kuwa mbio za farasi wawiili.
Chochote kile kitakachotokea, hizi
zitakuwa mbio za mwisho za Uhuru Kenyatta mtoto wa rais wa kwanz wa Kenya dhidi
na Raila Odinga ,mtoto wa makamu wa kwanza wa raia wa Kenya.
Kenyatta mwenye umri wa miaka 55 anataka
kuingoza kwa muhula wa pilia na wa mwisho kupitia chama cha Jubilee baada ya
kushinda uchaguzi wa mwaka 2013, licha ya kukabiliwa na kesi kwenye mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.Bwana Kenyatta ambaye anatoka jamii ya Kikuyu na hasimu wake wa zamani William Ruto kutoka jami ya Kalenjin, walilaumiwa kwa kuchochea ghasia kati ya jamii hizo.
Mashtaka yao yalihusiana na ghasia za baada ya Uchaguzi wa 2007 ambapo karibu watu 1200 waliuawa na kuwalazimu wengine maelfu kuhama makwao.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.