0
Basi la kampuni ya Sharon lililokuwa litatoka Dodoma kwenda Arusha, limepinduka eneo la mabanzini-Bohay mjini Babati na kusababisha vifo vya watu wawili huku wengine wakijeruhiwa.

Majeruhi wa ajarili hiyo wamepelekwa hospitali ya Mrara mjini Babati kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara Francis Masawe akizungumza juu ya ajali hiyo amesema kondakta na mtoto mdogo ndiyo walifariki.
Hata hivyo waliofariki bado hawajafamika kwa majina.
Chanzo cha ajali hiyo ni kona kali zilizopo kwenye bara bara bara hiyo inayofanyiwa matengenezo.
Aidha kamanda amesema  atazungumza na mamlaka zinazohusika na kutoa vibali ili waizuie bara bara hiyo kutumika kwani bado kwa sasa haipo vizuri kwa magari kupita haswa ya abiria.
Katika hatua nyingine ameuambia mtandao huu kuwa ajali ndani ya mkoa wa Manyara zimepungua kwa kiwango kikubwa bila kutaja ni kwa asilimia ngapi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top