Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi amewataka wadau mbalimbali wakiwemo
wazazi,walimu,viongozi wa dini na
mashirika kuelekeza juhudi zao katika kutokomeza tatizo la mimba za utotoni.
Mushi ameyasema hayo katika kampeni za kupinga ndoa za
utotoni iliyoandaliwa na Shirika lisilo la serikali WORL VISION TANZANIA
iliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Babati jumatano ya wiki hii
desemba 6 mwaka huu.
Sambamba na hayo jamii imeaswa kutokushiriki katika vitendo
vinavyochochea ndoa za utotoni badala yake kuwajenga watoto katika maadili mema ya kimwili na kiroho.
Mushi ameeleza kuwa serikali ipo tayari kushirikaina na
mashirika binafisi ktika jitihada za kukabiliana na tatizo la mimba za utotoni
ambalo limekuwa likikatisha ndoto zao.
mratibu wa shirika la WORLD VISION wilaya ya Babati Jesca
Mnana amesema wao wamedhamiria kwa kipindi cha muda wa miaka mitano kumaliza
tatizo la Mimba za utotoni kwa kutoa elimu watoto kuweza kujilinda kuepuka ndoa
hizo za utotoni pamoja na kuhakikisha sera za watoto zinatekelezwa.
‘World Vision kupitia kampeni hiyo inataka kuhakikisha
vijana na watoto wanapata stadi za Maisha ikiwemo elimu ya afya ya uzazi’
Kwa upande wa mratibu wa mradi wa ADP Magugu unaosimamiwa na
World Vision alisema kuwa ulinzi na usalama wa mtoto ni wajibu wa kila mtu na
kwamba kupitia shirika hilo wanaelimisha jamii juu yua haki,ustawi wa mtoto na
wajibu wa mzazi au mlezi katika kumlea na kumlinda mtoto.
Alisema watoto wengi wanafanyiwa vitendo vya ukatili na
unyanyasaji na hivyo kusababisha kushindwa kufurahia utoto wao na kuwaletea
madhara makubwa ikiwemo kuathiri kisaikolojia huku akisema kuwa hilo
lisipokomeshwa litaongeza hali ya umaskini nchini nchini kuongezeka.
Hata hivyo katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliowashirikisha
viongozi mbalimbali wa serikali,siasa na dini ambao uliazimia kukomesha ukatili
katika wilaya ya Babati kwa kutengeneza mkakati wa kamati ya ulinzi na usalama
katika kata 12 kati ya 25 zitakazosaidia
kutokomeza ndoa hizo.
Aidha wadau hao waliishauri serikali kubadili sheria ya ndoa
ya mwaka 1971bili iendane na mazingira ya sasa na pia kuondoa mila kandamizi
ambazo baadhi hulazimisha ndoa za umri mdogo.
Post a Comment
karibu kwa maoni