0


Mwenyekiti huyo alisema wakati wa ujenzi, chupa hizo hujazwa udongo uliochekechwa na kufungwa vizuri, hivyo kutumika kwa ujenzi kwa kutumia udongo na saruji kiasi ili kushikanisha chupa, kama inavyokuwa katika ujenzi wa matofali.
Kwa mujibu wa wataalamu wa aina hiyo ya ujenzi, nyumba huwa imara, zinaweza kuhimili mtikisiko wa ardhi, moto lakini pia wakati mwingine hazipenyezi risasi kirahisi.
 Mbali ya kutumia chupa hizo katika ujenzi wa nyumba, wabunifu katika nchi mbalimbali wamekwenda mbali zaidi na kutumia chupa hizo kwa ujenzi, hutumika pia kama mapambo ya ndani, hujengea uzio wa nyumba, hutumia kujengea paa mahali pa kuhifadhia magari, hugeuzwa `shamba’ kwa kupanda mimea katika maeneo ya mijini, lakini wapo wanaojenga pia mabanda ya mifugo, kuwekea miswaki, kutengeneza maboti na kadhalika.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top