0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu ameagiza kuwekwa ndani Afisa Mazingira Wilaya ya Biharamulo Michael MKuti kwa siku mbili kutokana na uzembe anaouonyesha katika kutekeleza majukumu ya Idara yake.
Maagizo hayo ameyatoa akiwa wilayani Biharamulo kwenye ziara ya kikazi kukagua miradi ya maji ambapo amesema kuwa afisa huyo amekuwa akionyesha uzembe katika Idara yake hali iliyopelekea miradi mingi kukwama na kusababisha wananchi kukosa huduma zao kimsingi.
Aidha, ameongeza kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira katika Wilaya ya Biharamulo na Mkuti ameshindwa kuwachukulia hatua wanaosababisha uharibifu huku akishindwa kuonekana kazini kwa kusingizia kuwa anaumwa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top