Mkuu wa mkoa wa Manyara dr.Joel Nkaya Bendera anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima katika mkutano mkuu wa kumi wa Chama cha wafanyabiashara,wakulima na wenye viwanda mkoa wa Manyara [TCCIA]utakaofanyika mjini Babati siku ya jumatano ya wiki hii.
Akizungumzia mkutano huo afisa mtendaji wa Chama hicho Mwanahamisi Hussein amesema katika mkutano huo watazungumzia namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara.
Aidha Mwanahamisi ameeleza kuwa wakulima watahamasishana kuhusu kuinua na kuendeleza viwanda vilivyopo ndani ya mkoa pamoja na kuzindua Saccos ya wakulima itakayowasaidia kupata huduma kiurahisi.
Wanachama hao wanatoka katika Wilaya zote tano za mkoa wa Manyara,Kiteto,Mbulu,Hanang,Simanjiro na Babati.
Mkutano huu huwa unafanyika kila mwaka.
TCCIA ilianzishwa rasmi mwaka 1988.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.