0


Na Gharos Riwa—BUNDA 0768 44 33 15
BUNDA
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwalimu Lydia Bupilipili amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuwa tayari kwa mapokezi ya mbio za mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuwasili hivi karibuni.

Amesema hayo wakati akiongoza wananchi wa halmashauri ya mji wa bunda katika kutimiza agizo la Makamu wa Rais Samia suluhu Hasani ya wananchi wote kushiririki michezo kila jumamosi ya pili ya kila mwezi, ambapo amesaema kuwa  mwenge huo wa uhuru unatarajiwa kufika wilayani  hapa tarehe 23 Agost 2017 ambapo utazindua na kutembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali.

Bupilipili amesema wataupokea mwenge huo wa uhuru kisorya, na utapita kuangalia miradi ya serikali ikiwemo zahanati ya Nansimo,shule ya sekondari nansimo, kasahunga,bulamba na baadae Makongoro sekondari na hatimae mwenge huo utalala Nyamuswa.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya mwenge huo kulala  nyamuswa,  tarehe 24.8. 2017 mwenge huo wa uhuru utaingia halmashauri ya mji wa bunda na utapokelewa kisangwa ambapo baadae utaendelea kukimbizwa katika hospitali ya Manyamanyama na katika kikundi cha maji cha Stop Over , pia utatembelea kiwanda cha kutengeneza mikate Bunda Bekary na hatimae shule ya sekondari  ya wasichana  ya ACT ya kanisa la Angilikana, ambapo baada ya kutembelea miradi hiyo utalala mjini hapa katika eneo la standi mpya.

Hata hivyo ametoa wito kwa wakazi wote wa wilaya ya bunda kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mwenge huo kwa kuwa mwenge wa uhuru una hadhi ya Rais wa Nchi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top