Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya
Tunduru Mkoa wa Ruvuma wamefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati
wakichimba mchanga wa kujengea darasa walipokuwa kwenye mafunzo ya
vitendo.
Akizungumza
kwa njia ya simu na mwandishi wa ukurasa huu, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa mkoani Rukwa SACP Gemini Mushi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kwamba wanafunzi waliofariki ni Selina Selemani
Kazembe (12) wa darasa la tatu pamoja na Sofia Sillo (9) darasa la tatu
kwa kusema kuwa watoto hao waliangukiwa kwa kufunikwa na ukuta wa shimo
la mchanga ambao ulikuwa ukitumika kujengea darasa.
Kamanda Mushi amefafanua kwamba "Kwa
mujibu wa taarifa tulizopewa na uongozi wa shule hiyo wanafunzi hao
walikuwa katika mafunzo ya vitendo yajulikanayo kama elimu ya
Kujitegemea (EK).
Pamoja na hayo Kamanda huyo amesema
jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza watoto hao katika hospitali ya
Mbesa lakini kwa bahatI mbaya wakati watoto hao wanafikishwa hospitali
walikuwa wameshakata roho.
Kwa mujibu wa Kamanda Mushi amesema jukumu la mazishi familia hizo zimeachiwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni