Mahakama ya Rufani Tanzania imebariki Uchaguzi mdogo wa ubunge katika
Jimbo la Longido mkoani Arusha kurudiwa baada ya kutupilia mbali rufaa
iliyokatwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Onesmo Ole Nangole kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Ole Nangole alikata rufaa hiyo dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk
Stephen Kiruswa ya kupinga hukumu iliyotolewa Juni 29, mwaka jana katika
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Jaji Sivangilwa Mwangesi aliyeamuru
uchaguzi urudiwe kutokana na upungufu uliyojitokeza.
Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Ester
Mkwizu alisema mahakama hiyo imetupa rufaa hiyo kwa kuwa ina upungufu wa
kisheria baada ya kukosekana kwa kielelezo namba nne na namba nane
kwenye kumbukumbu ya rufaa.
Kwa mujibu wa Wakili wa Dk Kiruswa,
Edmund Ngemela alidai mahakama imekubaliana na hoja za wajibu rufani
kuwa ili mahakama ipitie ushahidi upya uliotolewa mbele ya Jaji
Mwangesi, kwamba vielelezo vikikosekana ni lazima itupiliwe mbali.
Dk Kisurwa ambaye aliwakilishwa na
mawakili Ngemela, Dk Masumbuko Lamwai na Daudi Haraka, alipinga matokeo
ya uchaguzi yaliyompa ushindi Nangole katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015, kwa hoja za kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya
walioletwa na Ole Nangole.
Pamoja na madai hayo ilidaiwa pia
Chadema ilitumia magari kusindikiza na kubeba masanduku ya kupigia kura,
Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM
kutolewa nje na kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo.
Aidha kutokana na madai hayo, Jaji
Mwangesi aliamuru kwamba kwa kuzingatia kanuni, sheria na ushahidi
uliotolewa mahakama imetengua shauri hilo na kwa kujiridhisha kwamba
mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi
urudiwe upya.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimeshatangaza kujiweka sawa kwa uchaguzi huo mdogo utakaofanyika baada
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza tarehe
Post a Comment
karibu kwa maoni