0
Katika hali isiyo ya kawaida uchaguzi wa mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa ccm [UVCCM] Babati mjini mkoani Manyara umerudiwa mara tatu baada ya kura za wagombea kufanana mara mbili mfululizo.

Awali wagombea Hango Shabani Gwelo pamoja na Hassan Mdinku walifungana kwa kura 54-54 wakati awamu ya pili walipishana kwa kura moja 54-53, japo kwa kanuni za uchaguzi wa Ccm mshindi anatakiwa apate zaidi ya kura 54 hivyo uchaguziu ukarudiwa kwa mara ya tatu ambapo mshindi alipatikana kwa kura 57 ambaye ni Hassan Mdinku huku anayemfuatia Hango Shabani akiwa na kura 50.

Hassan Mdinku mwenye umri wa miaka 18 pekee anakuwa mwenyekiti wa Uvccm mwenye umri mdogo kuliko viongozi wote nchini  Tanzania.

Anasema ndoto yake kubwa ni kuja kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top