0
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Husein Mwinyi ameliambia Bunge kuwa kwa sasa kimeundwa kikosi kazi kwa ajili ya kusaka silaha za kivita ambazo zinatumiwa na watu wenye nia mbaya.
Dk.Mwinyi ametoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Chambani,Yusufu Salim Husein(CUF).
Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua serikali inachukua hatua gani ili kuweza kuthibiti kuzagaa kwa siraha za kivita ambazo zinaonekana kutumika vibaya kwa kuwajeruhi watu mbalimbali.
“Tunajua kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ndilo lenye jukumu la mipaka ya nchi ya kimataifa, sina shaka na usalama wa Mipakana,lakini ndani ya nchi hakuko salama je kuna utaratibu gani ambao unatumika kwa kuzagaa kwa silaha za kivita ambazo zinatumiwa kuwadhuru watu”alihoji Hussein.
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Mkoani, Twahir Awesu Mohamed(CUF) alitaka kujua serikali imejipanga vipi kuimarisha amani hapa nchini.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top