Mwanafunzi wa sekondari ambaye mpaka sasa haijafahamika ni wa shule gani huko wilayani Kondoa mkoani Dodoma amejifungulia kichakani na kukatelekeza kachanga.
Taarifa zinadai kuwa binti huyo anaedhaniwa kuwa na umri wa miaka 17 akiwa safarini kwenye gari kampuni ya Master Safari kutoka Irangi walipofika Bereko alidai kuwa amezidiwa tumbo linauma ndipo alipoteremka na kwenda katika kichaka hicho kisha kujifungua na kufunika kichanga hicho na Majani.
Wakati akifanya vile kuna msamaria alimuona na ndipo akapoga kelele na watu kukusanyika kukashuhudia kichanga.
Shuhuda alietoa taarifa kwenye mtandao huu anaeleza kuwa walifanikiwa kusimamisha gari na walipokagua walimgundua mwenye mtoto huyo kwani hali yake ilijulisha wazi kuwa yeye ndie mhusika.
Hata hivyo mtoto huyo ni mzima na amekabidhiwa msichana huyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni