Mfanyabiashara
Yusuf Manji ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo September 9,
2017 kuwa yeye bado ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu na kudai kuwa
hatambui kuvuliwa udiwani kama ilivyotangazwa na Mstahiki Meya wa
Temeke, Abdallah Chaulembo September 6, 2017.
Manji
ametoa malalamiko hayo, kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili na
wenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo katika kesi
hiyo ambayo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai
upelelezi haujakamilika na Manji kudai ameona habari kupitia gazetini
kuwa amevuliwa udiwani.
Amedai kama ni kweli amevuliwa Udiwani hatambui, kwani ana miezi 2 yupo gerezani na serikali inatambua kwamba yeye ni Diwani.
"Vikao
vya awali vya udiwani wa Halmashauri ya Temeke nilikuwa nahudhuria kwa
kuwa naheshimu Mahakama na kwa uzito wa hii kesi sikutaka kupeleka hata
maombi ya dhamana Mahakamani. Mahakama imuagizie DPP na aiambie
Halmashauri ya Temeke kwamba wamenikamata na ndio sababu ya kutohudhuria
vikao. Kama wanataka nihudhurie DPP aombe remove order nitolewe
gerezani ili niende kwenye vikao.”
Pia
Manji amedai kuwa kama hilo haliwezekani, basi wamuandikie barua
itakayoonyesha agenda ya vikao vyote na yeye atazijibu kwa njia ya barua
pia.
"Ninachotambua
mimi ni Diwani wa Mbagala Kuu na kama nimevuliwa au sijavuliwa udiwani
sitambui. Tayari nimetumia fedha zangu mwenyewe zaidi ya Tsh. Milioni 70
sio za Halmashauri kwa ajili maendeleo ya wananchi wake.”
Aidha,
amedai kuwa hiyo kesi ni nzito na DPP hapaswi kuangalia upande wake wa
kesi tu, kwani yeye amechaguliwa na wananchi na anawasaidia.
Awali
kabla ya kuelezwa hayo, Wakili wa utetezi Seni Malimi alidai kuwa
wanatarajia kuwasilisha maombi ambayo ni ya siri katika tarehe ijayo.
Baada
ya kuelezwa hayo, Hakimu Huruma Shaidi akautaka upande wa mashtaka
kuhakikisha wanalifanyia kazi suala hilo, ambapo kesi imeahirishwa hadi
September 18, 2017.
Post a Comment
karibu kwa maoni