Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefunguka na kusema watu
ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga risasi Mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Lissu wanaweza patikana ikiwa wananchi watasaidia jeshi hilo
kupata taarifa za wahalifu hao.
IGP
Sirro amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari akielezea
hali ya usalama wa nchi na kudai usalama wa nchi upo vizuri na kuwa
mpaka sasa jeshi la polisi limeongeza nguvu ya upelelezi mjini Dodoma
ili kuhakikisha linawapata watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga
risasi mbunge Tundu Lissu , huku akiwataka wananchi wasihusishe tukio
hilo na masuala ya kisiasa.
"Naomba
wananchi wasidanganywe kwenye suala zima la siasa na vitu vingine hapa
huwa nasema siku zote kama hakuna amani na usalama siasa haiwezi kupata
nafasi
"Hili
tukio limetokea tunapeleleza na tupo makini na hili tukio, kwa sasa
tumeongeza vikosi vya upelelezi Dodoma, wale waliofanya lile tukio ni
lazima tutawakamata ila upelelezi huu unaweza kuzaa matunda mazuri zaidi
endapo wananchi watatupa ushirikiano wa kutosha" alisema IGP Sirro
Aidha
IGP Sirro amezungumzia kuhusu moja ya kauli ya Tundu Lissu ambayo
aliwahi kusema kuwa kuna watu wanamfuatilia na kuvitaka vyombo vya
usalama kuacha kuwatuma watu hao kumfuatilia na kudai kuwa hakuwahi
kuripoti katika kituo chochote cha polisi, na kusema sasa usiwe wakati
wa kuzungumzia jambo hilo.
IGP
Sirro alimalizia kwa kusema kuwa jeshi la polisi lipo imara na lipo kwa
ajili ya kulinda watanzania pamoja na mali zao na si kuwamumiza
watanzania hivyo ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi
kuwapata watuhumiwa hao.
Post a Comment
karibu kwa maoni