Utafiti unaonyesha kuwa Kila mwaka asilimia 27 ya watanzania hupoteza maisha kutokana na magonjwa yasiyoambukiza yakiongoza magonjwa ya Sukari ,presha na saratani.
Hili ni
ongezeko kubwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa chama kinachopambana na magonjwa yasiyoambukiza
[TANCDA]mkoani Manyara Nickodemus Gaudence
wakati wa kutoa huduma za vipimo na
matibabu bure katika Zahanati binafsi ya Margakan iliyopo Babati mjini.
Dk
Nikocdemus ameiomba Serikali isaidiane na shirika la TANCDA ili kuondokana na
matatizo haya yanayowakabili wengi haswa tatizo la uzuzi kwa wanawake.
Kutokana na
kubainika kuwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na ngono na
mwanamke au mwanume ziadi ya mmoja Dk
Nickodemus ameshauri kuwa na mwenza
mmoja.
Shirikisho
la vyama vya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa Tanzania inayohusika na magonjwa
yasiyoambukiza TANCDA kwa kushirikiana na Zahanati ya Margakan Tanzania tawi la
Babati limetoa huduma za upimaji magonjwa bure
Nao wakina
mama wameeleza kufurahishwa kwao na huduma hizo za vipimo bure vya magonjwa na
kuitaka serikali ianzishe utaratibu huo ili kuwanusuru wakina mama na madhara
yatokanayo na Saratani ya kizazi.
Kutokana na
magonjwa hayo kutibiwa kwa gharama kubwa mfuko wa bima ya afya NHIF wamewataka
wananchi kujiunga katika mfuko huo kwa kukata kadi ya matibabu na kuokoa kiasi
kikubwa cha fedha za kutibiwa.
Charles
Nyawaga yeye ni afisa wanachama mfuko wa bima ya afya mkoa wa Manyara anasema
wameshatoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na kadi yua matibabu mkoa mzima na
wanaendelea kuwashawishi wananchi kujiunga.
Post a Comment
karibu kwa maoni