Aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Francis Jacob Masawe amewapongeza askari polisi wanawake wa mkoa huu kwa kuonyesha uwezo mkubwa katika majukumu yao.
Kamanda Masawe ameayasema hayo wakati wa hafla ya
kufunga maadhimisho ya miaka 10 ya
mtandao wa polisi wanawake Tanzania [TPF-NET]kwa mkoa wa Manyara yaliyofanyika
mjini Babati katika hotel ya white Rose ambayo yalianza Oktoba 10 2017-14-2017.
Katika kipindi cha maazimisho hayo askari hao wanawake
walitoa elimu kwa jamii ikiwemo mashuleni kupitia kitengo cha dawati la jinsia
na watoto kwa wilaya zote tano ambapo jumla ya watu wazima 6,085,000 wamepata
elimu kwa njia ya semina ,vikao huku watoto wapatao 405,000 wakipatiwa elimu
kwa shule za msingi na sekondari.
Taasisi ambazo dawati la jinsia limeshirikiana mkoani
Manyara ni World Vision,ustawi wa jamii wilaya na mkoa,Paralegal,Kanisa
Katoliki jimbo la Mbulu,MAHOSE,NAFGEM,REDIO MANYARA pamoja na MWEDO.
Aidha katika
kuonyesha uwezo wao katika kazi,askari hao wa kike walipangwa
sehemu mbalimbali za ulinzi kwenye mabenki ,kufanya mazoezi ya
kivita,kulinda kituo huku wakiongozwa na Askari Insekta Pilly katika mazoezi.
Naye kamanda wa kikosi cha usalama Bara barani mkoa wa
Manyara Mary Kipesha aliwataka askari hao wanawake wake za askari kushirikiana
kwa pamoja katika kufichua vitndo vya kikatili vinavyofanywa katika jamii hata
kama vinafanywa na askari wenyewe.
Askari hao wa kike katika risala yao kwa Kamanda Masawe
wamesema kuwa yapo mengi wameyafanya katika kipindi cha maazimisho hayo huku
wakisisitiza kuwa bado wana Ari ya kuchapa kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya
juu kwa kuzingatia kuwa mtandao huo ni mojawapo ya maboresho ya jeshi la
Polisi hivyo wanaendelea kuchapa kazi
huku wakiipigilia msumari kauli ya Rais John Pombe Magufuli ‘HAPA KAZI TU”.
Mtandao wa polisi
wanawake Tanzania ulianzishwa rasmi mwaka 2017 na aliyekuwa IGP
Kipindi hicho Said Mwema baada ya
kuona nchi zingine zina mtandao huo na
zinafanya vizuri katika majukumu yao,na askari wote wanawake ni wanachama wa
mtandao huo.
Mtandao huo ulianzishwa kwa madhumuni ya kuimarisha ulinzi
na usalama wa watu na mali zao jambo ambalo ndio msiongi wa askari polisi kwa
ujumla.
Mkoa wa Manyara una askari wanawake 232 kwa wilaya zote
ambazo ni Babati,Mbulu,Hanang,Simanjiro na Kiteto.
Post a Comment
karibu kwa maoni